Kaya Ramani

Kiswahili English
Sauti ya wakulima, "The voice of farmers", ni msingi wa kuelimishana ulioundwa na wakulima wa eneo la Chambezi Wilayani Bagamoyo-Tanzania. Msingi huu wa kuelimishana umeundwa kwa kukusanya ushahidi wa picha za shughuli zinazofanywa na wakulima kila siku na rekodi za sauti zao kisha kurekodiwa kwa kutumia ‘smartphones’ na kuchapishwa kwenye mtandao.

Washiriki wa Sauti ya wakulima ni kundi la wanaume watano na wanawake watano ambao hukusanyika kila Jumatatu katika kituo cha kilimo kilichopo Chambezi. Wao hutumia kompyuta ndogo iliyounganishwa na mtandao wa mawasiliana wa 3G ili kuona picha na kusikiliza sauti zilizorekodiwa na kuchapishwa kwenye mtandao kwa kipindi cha wiki hiyo. Wao pia hukabidhi ‘smartphones’ mbili zilizopo katka kikundi toka kwa washiriki fulani kwenda kwa washiriki wengine, ili nao waweze kuzitumia kama zana za mawasiliano kati yao. Smartphones hizi zimeunganishwa na vifaa vingine kama vile viunzi huru vya GPS na vibandiko vingine ambavyo kwa pamoja hurahisisha utumaji wa picha na sauti kwenye mtandao. Wakulima hawa wa Chambezi huzitumia ‘smartphone’ hizi kurekodi/kuratibu shughuli zao za kila siku, kutoa taarifa juu ya masuala yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na pia kufanya mahojiano na wakulima wengine, hivyo kupanua mtandao wa mahusiano ya kijamii kati yao.

Mbali na kupambana na ubovu wa miundo mbinu/kutokuwa na miundo mbinu ya kutosha na na hali ya kutokuwa na masoko ya huhakika kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao, wakulima wa Chambezi pia wanakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Pamoja na hayo, uhaba wa mvua, uhaba wa maji yanayopatikana chini ya ardhi na vitisho visivyo na kifani vivyosababishwa na wadudu na magonjwa ya mimea ni miongoni mwa masuala makubwa ambayo wakulima hawa wanalazimika kushughulikia. Hata hivyo, wakulima hawa wanatambua ya kuwa kwa kushirikishana maarifa wanayotumia katika kukabiliana na matatizo haya wanaweza kuwa na nguvu na kutafuta njia mbadala za kukabiliana nayo. Pia wakulima hawa wana matumaini kwamba, kwa kuwasilisha uchunguzi wao kwa maofisa ugani na watafiti wa kisayansi ambao wapo mbali nao wanaweza wakashirikiana nao katika kubuni mbinu mpya kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo. Wanataka sauti zao kusikika; wanayo mengi sana ya kuzungumza/kusema.

Kupata sisi katika Envaya.orgShukrani kwa:

Wakulima: Abdallah Jumanne, Mwinyimvua Mohamedi, Fatuma Ngomero, Rehema Maganga, Haeshi Shabani, Renada Msaki, Hamisi Rajabu, Ali Isha Salum, Imani Mlooka, Sina Rafael

Mratibu wa kikundi/afisa ugani: Mr. Hamza S. Suleyman

Washauri wa kisayansi: Dr. Angelika Hilbeck (ETHZ), Dr. Flora Ismail (UDSM)

Programming: Eugenio Tisselli, Lluís Gómez i Bigorda

Tafsiri: Cecilia Leweri

Msanifu: Joana Moll, Eugenio Tisselli

Mradi umeletwa na: Eugenio Tisselli, Angelika Hilbeck, Juanita Schläpfer-Miller

Umedhaminiwa na: The North-South Center, Swiss Federal Institute of Technology - Zurich (ETHZ)


Kwa msaada wa:
The Department of Botany, University of Dar es Salaam (UDSM)

Z-Node: The Zurich Node of the Planetary Collegium. Institute of Cultural Studies, University of Applied Arts, Zurich


Sauti ya wakulima ni msingi katika mradi megafone.net

Move Commons Non-Profit, Reproducible, Reinforcing the Ecology Commons, Representative

Move Commons Non-Profit, Reproducible, Reinforcing the Ecology Commons, Representative


Creative Commons License
The audiovisual content of Sauti ya wakulima by Sauti ya wakulima is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 Unported License